Book cover

Naenda Na Yesu

Nyimbo za Ziada kwa ajili ya Watoto

0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Yesu alikua, Nayo hekima, Na upendo kwa watu kaonyesha. Anielekeza, Njia nipate, Akiniita nitembee naye.

Naenda na Yesu Mbinguni huko, Bwana atanibariki, Niwe na upendo. Anibadilisha; Nipate maoni. Naenda na Yesu, Ataenda nami.

2. Nitamwiga Yesu. Nitajaribu Kuzitii amri kila siku. Nitakaa naye Akinilinda, Nitakuwa naye kumtangaza.

Naenda na Yesu Mbinguni huko, Bwana atanibariki, Niwe na upendo. Anibadilisha; Nipate maoni. Naenda na Yesu, Ataenda nami.

3. Nitamuamini; Nitaitika. Hataniacha hata nikikosa. Ananipa nguvu, Anifariji, Milele nikikua na kuishi.