1. Tusonge mbele kwenye kazi ya Bwana, Ndipo tukaipate zawadi tukifa; Katika vita tuushike upanga, Upanga wa ukweli.
Jipe moyo shinda adui Msihofu, Bwana yu nasi Hatutawasikiliza waovu Tutamtii Bwana Mungu.
2. Hatutasita ingawa tu wachache Tunapolinganishwa na adui kule; Katika Bwana nguvu yake tupate Kutetea ukweli.
Jipe moyo shinda adui Msihofu, Bwana yu nasi Hatutawasikiliza waovu Tutamtii Bwana Mungu.
3. Hatutahofu tunapotenda mema, Kwa sababu Bwana yu karibu daima; Katika shida yeye atuwezesha Tuushike ukweli.
Jipe moyo shinda adui Msihofu, Bwana yu nasi Hatutawasikiliza waovu Tutamtii Bwana Mungu.