1. Nje ya Yerusalemu Kilimani kule, Alisulubiwa Kristo Kuokoa sote.
2. Hatuwezi kuelewa Yake maumivu, Aliteswa, twaamini, Kwa ajili yetu.
3. Hapakuwa na mwingine, Wa kulipa deni. Yeye kafungua lango Tufike mbinguni.
4. Alitupenda kwa dhati! Nasi tumpende! Damu yake tusadiki, Na tumfuate.