1. Kwa unyenyekevu, Bwana, Twaomba Roho wako. Twabariki sakramenti Katika jina lako. Mwokozi sitasahau Ulivyo sulubiwa, Ulivunjwa moyo wako Juu ya msalaba.
2. Tuwezeshe kusamehe, Tuwe wavumilivu. Sala zetu zije kwako Juu patakatifu. Iwapo tutastahili, Dhabihu takatifu, Twakuomba tuwe nawe; Tuwe na utukufu.