1. Ukweli ni nini? Thamaniye Huzidi vito na dhahabu, Na ubora utaonekana pale Ambapo utajiri wote wa falme Utaonwa kama uchafu.
2. Ukweli ni nini? Tuzo zuri Watu na mbingu kuwania. Utafute ung’aripo kilindini, Au ufukuzie hadi mbinguni: Ni lengo la kutamaniwa.
3. Mwonevu nguvu atazidiwa Ataposhindana na haki. Hivyo ukweli utadumu daima, Na ngome yake kuhimili vimbunga Na mapinduzi ya katili.
4. Hivyo, ukweli ni mwisho na mwanzo, Msimu, nyakati hauna. Japo mbingu, nchi zitafika mwisho, Ukweli, uhalisi, utakuwepo, Kubakia hivyo, daima.