Book cover

Kuna Upendo Kila Mahali

Nyimbo Za Dini Pamoja Na Nyimbo Za Watot, 42


1. Kuna uzuri kote Penye upendo; Furaha ipo tele Penye upendo. Amani na neema, Zabubujika hapa. Muda wote ni raha Penye upendo. Upendo, nyumbani; Muda wote ni raha Penye upendo.

2. Nyumbani kuna shangwe Penye upendo; Hakuna chuki kamwe Penye upendo. Waridi zinastawi; Dunia ni bustani, Maisha huwa heri, Penye upendo. Upendo, nyumbani; Maisha huwa heri, Penye upendo.

3. Mbingu hutabasamu Penye upendo; Dunia ni karimu Penye upendo. Mito hutuimbia; Angani kunang’aa. Mungu naye apenda Penye upendo. Upendo, nyumbani; Mungu naye apenda Penye upendo.