1. Ulipoamka leo, Je, uliomba? Katika jina la Kristo, Kusihi upendeleo Ili kulindwa?
Jinsi sala hufariji! Nuru huongezeka. Punde ukiwa gizani, Kumbuka sala.
2. Ulipopata hasira, Je, uliomba? Upewe neema, ndugu, Wengine usihukumu, Waliokosa?
Jinsi sala hufariji! Nuru huongezeka. Punde ukiwa gizani, Kumbuka sala.
3. Ulipopatwa na shida, Je, uliomba? Ulipojawa huzuni, Malhamu ya Gileadi Ulitafuta?