1. Usiku mtulivu! Ku kimya, ku ng’avu Kote kwa mama na Mwana. Mtukufu, Mwana mwanana, Lala kwa amani Lala kwa amani.
2. Usiku mtulivu! Mchunga ahofu! Utukufu watokea; Mbingu yaimba Haleluya! Azaliwa Kristo! Azaliwa Kristo!
3. Usiku mtulivu! Upendo mng’avu Wang’ara mwako usoni Na neema ya ukombozi, Waja Bwana Mungu. Waja Bwana Mungu.