Book cover

Bwana Kristo Amefufuka Leo

Nyimbo Za Dini Pamoja Na Nyimbo Za Watot, 50


1. Mwokozi amefufuka, Haleluya! Tuseme na malaika, Haleluya! Ushindi kwake juu, Haleluya! Imba dunia na mbingu, Haleluya!

2. Ukombozi ameleta, Haleluya! Na vita amevishinda, Haleluya! Yesu hana mateso, Haleluya! Na giza tena haliko, Haleluya!

3. Kristo tena anaishi, Haleluya! Nguvu ya kifo i wapi? Haleluya! Afa kutuokoa, Haleluya! Kaburi u wapi sasa? Haleluya!