Book cover

Njooni Enyi Watoto Wa Bwana

Nyimbo Za Dini Pamoja Na Nyimbo Za Watot, 12


1. Enyi wana wa Bwana, Tuimbe kwa umoja. Tupaze wetu wimbo Kwake atawalapo. Tutasafishwa wote, Na makosa yafutwe, Tutapoacha dhambi, Tuishi kwa amani.

2. Tutakavyofurahi Tumwonapo Mwokozi! Aja kwa utukufu, Kukomesha maovu. Nyimbo tutamwimbia Mfalme wetu, Bwana. Tutajaa upendo, Woga kufika mwisho!

3. Tutakuwa wasafi, Tutaishi nuruni. Tutamwimbia sifa; Shangwe tutazipaza. Dunia isafishwe Viumbe vyake vyote, Viishi kwa upendo; Furaha kila moyo.