Nyimbo Za Dini Pamoja Na Nyimbo Za Watot (1983),
p. 12
Njooni Enyi Watoto Wa Bwana
Njooni Enyi Watoto Wa Bwana
1. Enyi wana wa Bwana,
Tuimbe kwa umoja.
Tupaze wetu wimbo
Kwake atawalapo.
Tutasafishwa wote,
Na makosa yafutwe,
Tutapoacha dhambi,
Tuishi kwa amani.
2. Tutakavyofurahi
Tumwonapo Mwokozi!
Aja kwa utukufu,
Kukomesha maovu.
Nyimbo tutamwimbia
Mfalme wetu, Bwana.
Tutajaa upendo,
Woga kufika mwisho!
3. Tutakuwa wasafi,
Tutaishi nuruni.
Tutamwimbia sifa;
Shangwe tutazipaza.
Dunia isafishwe
Viumbe vyake vyote,
Viishi kwa upendo;
Furaha kila moyo.
Maandishi: James H. Wallis, 1861–1940
Muziki: Lahani ya Uhispania; umepangiliwa na Benjamin Carr, 1768–1831
Maandishi: James H. Wallis, 1861–1940
Muziki: Lahani ya Uhispania; umepangiliwa na Benjamin Carr, 1768–1831