Book cover

Kazi Ilivyo Tamu

Nyimbo Za Dini Pamoja Na Nyimbo Za Watot, 13


0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Kazi tamu, Mungu wangu,Jina lako kulisifu,Pendo lako kuonyesha,Ukweli wako kusema.

2. Siku tamu ya Sabato,Ya dunia niachapo.Nitaimba kwa uzuriKwa kinubi cha Daudi!

3. Moyo wangu utasifuKazi yako kushukuru.Neema yako yang’ara!Wosia wako, hekima!

4. Ni ushindi uliojeKwa jina lako milele,Kwa furaha nikionaUso wako uking’aa!

5. Sitasumbuliwa kamweNa dhambi, adui yule,Maadui watashindwa,Shetani hatasumbua.

6. Na kisha nitayapataYote niliyoyataka,Nitafanya kila kituMilele mbinguni juu.