1. Ee Baba wa milele, Uliye mbinguni, Katika jina Lake, Takasa, bariki— Ikiwa tu wasafi— Mkate, divai, Ili tuikumbuke Damu nao mwili.
2. Dhabihu takatifu Tusiyoelewa, Kusamehewa dhambi, Na kumkumbuka, Ili tushuhudie Kuteswa kwa Kristo, Tuwe na Roho wake, Na upatanisho.
3. Na Yesu, Mteule, Akashuka chini Kujitoa dhabihu Kuokoa nafsi— Asiye na mvuto, Wa kutamaniwa— Mwokozi wa ahadi Akatutakasa.
4. Ile hekima kuu, Mpango kamili Ulifanya wokovu, Neno kuwa mwili, Kushuka duniani Awe mwanadamu, Afe, japo Mfalme, Kutuweka huru.