Book cover

Yesu Alizaliwa Kimaskini

Nyimbo Za Dini Pamoja Na Nyimbo Za Watot, 19


1. Mzaliwa horini, Sasa ni Mkombozi. Mwanzo aliteseka; Sasa ni Mtawala. Sasa ni Mtawala.

2. Mwanzo mwana kondoo, Sasa ni “MIMI NIKO”. Alionja mauti; Sasa yu mawinguni. Sasa yu mawinguni.

3. Alitokwa na damu, Sasa yu mtukufu. Aliyepingwa kwao; Sasa Mfalme wao. Sasa Mfalme wao.

4. Aliachwa mpweke, Sasa enzi ni yake. Yote alibebeshwa; Sasa habebi tena. Sasa habebi tena.