Page 19
Yesu Alizaliwa Kimaskini
Yesu Alizaliwa Kimaskini
1. Mzaliwa horini,Sasa ni Mkombozi.Mwanzo aliteseka;Sasa ni Mtawala.Sasa ni Mtawala.
2. Mwanzo mwana kondoo,Sasa ni “MIMI NIKO”.Alionja mauti;Sasa yu mawinguni.Sasa yu mawinguni.
3. Alitokwa na damu,Sasa yu mtukufu.Aliyepingwa kwao;Sasa Mfalme wao.Sasa Mfalme wao.
4. Aliachwa mpweke,Sasa enzi ni yake.Yote alibebeshwa;Sasa habebi tena.Sasa habebi tena.
Maandishi: Parley P. Pratt, 1807–1857
Muziki: Giacomo Meyerbeer, 1791–1864, umefanyiwa marekebisho