Book cover

Ninashangaa Sana

Nyimbo Za Dini Pamoja Na Nyimbo Za Watot, 16

1. Nastaajabu upendo wa Yesu kwangu, Nashangaa neema yake timilifu. Yasisimua kwamba alisulubiwa, Kwa ajili yangu, aliteswa na kufa.

Ni ajabu kwangu angenithamini Kiasi cha kufa! Ni ajabu kwangu, ajabu sana!

2. Nastaajabu kwamba angetoka juu Kuokoa nafsi kiburi kama yangu, Kwamba upendo wake angenionesha, Kunikomboa, hata kunihalalisha.

Ni ajabu kwangu angenithamini Kiasi cha kufa! Ni ajabu kwangu, ajabu sana!

3. Nawaza mikono yake ilivyochomwa! Nisahauje upendowe na huruma? Hata! Nitamtukuza na kumsifu, Hadi miguuni nitapomsujudu.

Ni ajabu kwangu angenithamini Kiasi cha kufa! Ni ajabu kwangu, ajabu sana!