Nyimbo Za Dini Pamoja Na Nyimbo Za Watot (1983),
p. 16
Ninashangaa Sana
Ninashangaa Sana
1. Nastaajabu upendo wa Yesu kwangu,
Nashangaa neema yake timilifu.
Yasisimua kwamba alisulubiwa,
Kwa ajili yangu, aliteswa na kufa.
Ni ajabu kwangu angenithamini
Kiasi cha kufa!
Ni ajabu kwangu, ajabu sana!
2. Nastaajabu kwamba angetoka juu
Kuokoa nafsi kiburi kama yangu,
Kwamba upendo wake angenionesha,
Kunikomboa, hata kunihalalisha.
Ni ajabu kwangu angenithamini
Kiasi cha kufa!
Ni ajabu kwangu, ajabu sana!
3. Nawaza mikono yake ilivyochomwa!
Nisahauje upendowe na huruma?
Hata! Nitamtukuza na kumsifu,
Hadi miguuni nitapomsujudu.
Ni ajabu kwangu angenithamini
Kiasi cha kufa!
Ni ajabu kwangu, ajabu sana!
Maandishi na muziki: Charles H. Gabriel, 1856–1932
Maandishi na muziki: Charles H. Gabriel, 1856–1932