1. Tenda mema; imeanza siku, Mwanga na uhuru vyaingia. Na malaika waandika juu Kila tendo, hivyo tenda mema.
Tenda mema; matokeo badaye. Kwa nguvu uhuru pigania; Kwa moyo shupavu uendelee. Mungu yupo, hivyo tenda mema!
2. Tenda mema; zafunguka pingu. Wafungwa uhuru wamepata. Kwa imani hawana maumivu. Ukweli wasonga; tenda mema.
Tenda mema; matokeo badaye. Kwa nguvu uhuru pigania; Kwa moyo shupavu uendelee. Mungu yupo, hivyo tenda mema!
3. Tenda mema; uoga uache. Songa mbele, lengo waliona. Nayo machozi yatakwisha punde. Kuna baraka kutenda mema.