Book cover

Mbali Katika Mbuga Za Judea

Nyimbo Za Dini Pamoja Na Nyimbo Za Watot, 48

1. Mbali kwenye nyanda za Yudea, Wachungaji walisikia:

Utukufu, Utukufu, Utukufu kwake Mungu. Amani duniani, Kwa watu pawe kwema.

2. Sauti za upendo mtamu, Ujumbe mwema kutoka juu:

Utukufu, Utukufu, Utukufu kwake Mungu. Amani duniani, Kwa watu pawe kwema.

3. Tufurahie na malaika, Tuimbe kwa moyo mmoja:

Utukufu, Utukufu, Utukufu kwake Mungu. Amani duniani, Kwa watu pawe kwema.

4. Siku hiyo ifike haraka Ambapo wote tutaimba: