1. Mimi mwana wa Mungu, Kanituma hapa, Kanipatia makao Na wazazi wema.
Niongoze, enda nami, Njia nipate. Nifunze la kufanya Nikaishi naye.
2. Mimi mwana wa Mungu, Nahitaji sana; Nielewe neno lake Kabla siku kwisha.
Niongoze, enda nami, Njia nipate. Nifunze la kufanya Nikaishi naye.
3. Mimi mwana wa Mungu, Baraka ni tele; Nikifanya apendavyo, Nitaishi naye.