Nyimbo Za Dini Pamoja Na Nyimbo Za Watot (1983),
p. 57
Mimi Ni Mtoto Wa Mungu
Mimi Ni Mtoto Wa Mungu
1. Mimi mwana wa Mungu,
Kanituma hapa,
Kanipatia makao
Na wazazi wema.
Niongoze, enda nami,
Njia nipate.
Nifunze la kufanya
Nikaishi naye.
2. Mimi mwana wa Mungu,
Nahitaji sana;
Nielewe neno lake
Kabla siku kwisha.
Niongoze, enda nami,
Njia nipate.
Nifunze la kufanya
Nikaishi naye.
3. Mimi mwana wa Mungu,
Baraka ni tele;
Nikifanya apendavyo,
Nitaishi naye.
Niongoze, enda nami,
Njia nipate.
Nifunze la kufanya
Nikaishi naye.
Maandishi: Naomi W. Randall, 1908–2001. © 1957 IRI
Muziki: Mildred T. Pettit, 1895–1977. © 1957 IRI
Maandishi: Naomi W. Randall, 1908–2001. © 1957 IRI
Muziki: Mildred T. Pettit, 1895–1977. © 1957 IRI