Book cover

Roho wa Mungu

Nyimbo za Dini, 2

0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Roho wa Mungu awaka kama moto! Utukufu wa zama hizi waja; Zarudi baraka za kale, maono, Na malaika wazuru dunia.

Tutaimba nao majeshi ya mbingu Hosana, hosana Mungu na Kristo! Utukufu wapewe walio juu Sasa na milele yote, Amina!

2. Bwana atuongezea ufahamu, Kama mwanzo, mwamuzi arejeshwa. Waongezeka na uwezo wa Mungu; Pazia linaanza kupasuka.

Tutaimba nao majeshi ya mbingu Hosana, hosana Mungu na Kristo! Utukufu wapewe walio juu Sasa na milele yote, Amina!

3. Kusanyiko la kiroho tutaita, Na kueneza ufalme wa mbingu, Kwa imani tutaanza kurithishwa Baraka na utukufu wa Mungu.

Tutaimba nao majeshi ya mbingu Hosana, hosana Mungu na Kristo! Utukufu wapewe walio juu Sasa na milele yote, Amina!

4. Siku ya ajabu watakapolala Kondoo na simba bila ghadhabu, Efrahimu Sayuni kutunukiwa, Kwa garimoto ashukapo Yesu!