Book cover

Mwokozi wa Israeli

Nyimbo za Dini, 6


0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Mwokozi wa Israeli, nuru yetu, Tunayemwomba baraka, Kivuli mchana; nguzo usiku, Mfalme, mwingine hatuna!

2. Twajua aja kukusanya kondoo Awaongoze Sayuni; Wasilie kwenye bonde la kifo Na wasizurure nyikani.

3. Tumetangatanga sana kwenye dhambi, Jangwani tukakuomba! Adui wabeza yetu majonzi, Lakini huru tutakuwa.

4. Habari njema kwetu wana Sayuni. Ishara zaonekana. Kwani ufalme ni wetu, tutii. Saa ya ukombozi yaja.

5. Nirejeshee, Mwokozi, nuru yako; Faraja ya roho nipe; Na ile shauku ya kuja kwako Moyo tumaini iipe.

6. Atazama! Na malaika wasifu, Wengi neno wangojea; Anena! Na anga zote za juu, Zazijibu sifa za Bwana.