1. Asante Mungu kwa nabii,Kutuongoza hizi siku.Asante kuleta injili,Iongezayo ufahamu.Asante kwa kila baraka,Pia kwa ukarimu wako.Twapenda kukutumikiaNa kuzitii amri zako.
2. Na shida zinapotuzonga,Na kutisha amani yetu,Matumaini hutujia,Kwamba wokovu u karibu.Hatuna mashaka kwa MunguNi dhahiri toka zamani.Hakika wataangamizwaWaovu wapinga Sayuni.
3. Tutamsifu siku zote.Rehema zake tutaimba,Tufurahie injiliye,Na mwangaza wenye uzima.Ukamilifu wa mileleWatapewa waaminifu,Wakanao injili hiiFuraha hawata fahamu.