Book cover

Mungu Mbariki

Nyimbo za Dini, 12


0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Mungu mbariki Mpendwa nabii, Mpe afya. Na utuongoze sote Kwa maneno yake, Ili tuchague Yale mema.

2. Na wako ufalme, Uenee pote Ufikapo. Ukweli wawaka, Nasi twaungana, Kwa kasi kufika Kwenye lengo.

3. Tuwe na umoja, Kama Baba, Mwana, Kwa amani. Kwa mioyo yote, Tusimame sote, Na milele tuwe Majasiri.