Book cover

Asubuhi Ile Njema

Nyimbo za Dini, 15


0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Asubuhi ile njema! Jua likachomoza. Na sauti zao ndege, Zote zilisikika. Hapo katika kisitu Joseph kamwomba Baba, Hapo katika kisitu Joseph kamwomba Baba.

2. Alipopiga magoti— Sala yake ya kwanza— Nguvu za Shetani nazo Zikamshambulia; Hakusita kuamini Mungu atamlinda, Hakusita kuamini Mungu atamlinda.

3. Ghafla mwanga ukashuka Unaozidi jua, Na mwale wa utukufu Ukammulikia, Ndipo wakaja wawili, Mungu Baba na Mwana, Ndipo wakaja wawili, Mungu Baba na Mwana.

4. “Huyu, Mwanangu Mpendwa; Utamsikiliza!” Kajibiwa sala yake, Akamtii Bwana. Ni furaha iliyoje, Kumwona Mungu Baba, Ni furaha iliyoje, Kumwona Mungu Baba.