1. Sifa kwa aliyenena na Bwana! Nabii huyo alitawazwa. Alifungua kipindi cha mwisho, Watamheshimu mataifa.
Shangwe kwa nabii kwenda mbinguni! Waasi sasa, bure wapinga. Akichangamana nao Miungu; Na kifo hakimshindi tena.
2. Atakumbukwa kwa kufia dini; Jina lake litaheshimiwa! Damu waliyoimwaga waovu, Kwake Mungu itamtetea.
Shangwe kwa nabii kwenda mbinguni! Waasi sasa, bure wapinga. Akichangamana nao Miungu; Na kifo hakimshindi tena.
3. Hauna mwisho ukuhani wake. Milele funguo amiliki. Ataingia katika ufalme, Kutuzwa kati ya manabii.
Shangwe kwa nabii kwenda mbinguni! Waasi sasa, bure wapinga. Akichangamana nao Miungu; Na kifo hakimshindi tena.
4. Dhabihu yatuletea baraka. Kote maovu yatajutiwa. Zindukeni tupiganie haki. Jina la Joseph litakumbukwa.