1. Tumpendao Mungu,Njooni kwa furaha.Tumwimbie nyimbo tamu,Tumwabudu pamoja.
2. Kuna wale wageniWasiojua neno.Sisi ndio watumishiWakutangaza kwao.
3. Mungu ni MtawalaWa dunia na mbingu,Kwa kauli hutulizaDhoruba na ghadhabu.
4. Huyu Mwenyezi Bwana,Ndiye upendo wetu,Nguvu zake atatumaKutupeleka juu.