1. Msafiri kwa miguuSafarini twakutana,Huomba nimnusuruSijaweza kumnyima.Hamu kujua si nayo,Atokako, aendako;Lakini machoni mwakeHuniteka na mboniye.
2. Nilipokuwa nakula,Akaja; pasipo hali,Akiwa na njaa sana,Nikampa; kabariki,Akala na akanipaTena, sikutegemea.Nilipokula kwa hamu,Kikawa kitamu kwangu.
3. Nikamuona mtoni;Hakuwa na nguvu kunywa.Yakitiririka maji,Kikombe nikakichovya.Nikamvuta karibu;Akanywa, tena kwa hamu.Mara ya tatu, kanipa;Nikanywa, kiu kukata.
4. Usiku baridi kaliNa upepo ukavuma.Nilisikia kwa mbaliSauti ilipoita.Nikajibu njoo kwangu.Nikampa mto wangu,Nikalala sakafuni,Nikahisi ni Edeni.
5. Kapigwa na kunyang’anywa,Katelekezwa njiani.Pumzi nikamhuisha,Na nikampa nusuri.Kwa huduma akapona.Shida zangu nikafichaNa hata kuzisahau;Amani ikanitibu.
6. Gerezani nikamwona,Kashtakiwa uhaini.Waongo niliwazima,Kwa hizo zao kejeli.Moyo wangu kujaribu,Akadai pumzi yangu.Mwili wabishia wito,Roho yaitika, “Ndiyo!”
7. Mara tu mwangu usoniAfichuka yule mtu.Alama zake si ngeni;Mwokozi yu mbele yangu.Ndipo akaniambia,“Nami haukuchukizwa.Huu ni wako urithi;Ulinitendea mimi.”
Maandishi: James Montgomery, 1771–1854
Muziki: George Coles, 1792–1858, umebadilishwa.
Wimbo uliimbwa kabla ya kifo cha kishahidi cha Nabii Joseph Smith. Tazama Historia ya Kanisa, 6:614–15.