1. Watakatifu mtii Mwamuzi mkuu. Andaa njia ya Bwana; Sasa yu karibu. Andaeni meza kuu, Wote waje kula. Tazama Bwana Harusi Aja kwa adhama.
2. Mwombeni Bwana kwa sala Ili wanadamu Waupokee ufalme Na wote wasifu. Funguo zimerejeshwa; Injili sambaza, Wekeni wazi ukweli Umefunuliwa.
3. Utukufu wake Bwana Wawaka Sayuni, Maana ndiyo mnara; Naye ni mlezi. Watakatifu fuata Nyayo za mababu. Kwa nyoyo za shukurani Tumuenzi Mungu.