1. Acha Sayuni ing’are;Nuruye yawaka.Ajapo Mfalme wake,Mbingu atagawa,Kote lienee nenoKuandaa watuKukutana na HenokoNaye Bwana juu.
2. Parapanda pulizeniMalaika wote.Taarifa sambazeniDuniani kote:Kwamba Yesu kwenye mbingu,Aja kuokoaWalio Watakatifu,Mwovu kuondoa.
3. Litaanza pumzikoLililotangazwa,Watakatifu na KristoWataitawalaMilenia duniani;Bwana, niandaeNikae nawe SayuniTusitenganishwe.