1. Sayuni nzuri mbinguni; Napenda mji mzuri; Mizuri milango yake; Hekalu – Mungu nuruye; Aliyenipatanisha, Milango aifungua.
A! Sayuni, ni kuzuri; Mji Sayuni; Sayuni, kwake Mungu!
2. Kuzuri mbinguni kote; Hata malaika wote; Nzuri nazo tumbuizo; Nzuri tarumbeta zao; Nitaimba na umati, Miguuni pa Mwokozi.
A! Sayuni, ni kuzuri; Mji Sayuni; Sayuni, kwake Mungu!
3. Mazuri mataji yao, Matawi watandazayo; Wazuri wakombolewa, Wote wanaoingia; Nitaingia kwa hamu Kwenye pumziko langu.
A! Sayuni, ni kuzuri; Mji Sayuni; Sayuni, kwake Mungu!