Book cover

Katika Siku ya Shangwe

Nyimbo za Dini, 24

0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Katika siku ya shangwe, Bwana, twakutukuza; Hapa ni patakatifu, Utukufu twaimba.

Haleluya, Haleluya, Sauti tuzitoe, Tuimbeni kwa furaha Kwa Bwana na Mfalme!

2. Ifungue chemichemi; Zimwagike baraka, Kwa wakutumikiao Kwenye hii dunia.

Haleluya, Haleluya, Sauti tuzitoe, Tuimbeni kwa furaha Kwa Bwana na Mfalme!

3. Tujenge ufalme wako, Alisema nabii, Kwamba wana wa ahadi Ndipo watapoishi.

Haleluya, Haleluya, Sauti tuzitoe, Tuimbeni kwa furaha Kwa Bwana na Mfalme!