1. Njoo, Ee Mfalme! Tumekungojea, Huru utufanye Kwa wako uweza. Njoo Ewe Mkombozi, Ukusanye Israeli.
2. Dhambi ukomeshe, Takasa dunia, Haki uilete, Tuweze kuimba, Nyimbo nzuri, kwa kinubi, Mfalme tukikulaki.
3. Hosana waimbe Waliookoka, Utukufu uje Kwa kuimba upya, Nyimbo nzuri za Sayuni Zitasikika mbinguni.
4. Karibu, Mfalme! Mahali pa enzi! Pale Wateule Watakapokiri, Na waasi kuabudu Ndimi zote zitasifu.