1. Msifu aliye juu,Bwana Mungu Muumba,Mwamba wa wokovu wetu,Chanzo cha mamlaka.Huniponya kwa upendoNa kuituliza roho.Sifa kwake milele!
2. Ayafanyayo kwa nguvuRehema yahifadhi.Asubuhi na usikuJichowe halilali.Katika ufalme wake,Haki hutawala kote!Sifa kwake milele!
3. Bwana yu karibu nasi,Kwenye zote taabu,Daima ndiye auni,Amani na shauku.Kama upendo wa mama,Aongoza wake wana.Sifa kwake milele!
4. Hivyo, katika taabuNaimba sifa zako,Ili wasikie watuNakuimbia wimbo.Moyo, furahia Bwana,Nawe nafsi, mwili pia!Sifa kwake milele!