1. Kwa nyimbo za utukufu, Twamwabudu Bwana, Twampatia shukrani Kwa kutukomboa.
Njoo mbele za Mungu! Mfanye ibada! Semeni haja za moyo Hata kwa kuimba.
2. Wimbo wa waadilifu Ni sala kwa Bwana; Wamkaribisha Roho, Watujumuisha.
Njoo mbele za Mungu! Mfanye ibada! Semeni haja za moyo Hata kwa kuimba.
3. Hapo kale Ibrahimu Aliimba nyimbo; Wimbo mpya tutaimba Akirudi Kristo.