Book cover

Sifa Kwa Bwana, Mwenyezi

Nyimbo za Dini, 33


0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Sifa kwa Bwana, Mwenyezi, Mfalme wa mbingu!O! Nafsi msifu aliye wokovu wangu!JumuikaKwa zeze na kinanda,Imbeni kwa kumwabudu!

2. Sifa kwa Bwana! Atawala kwa utukufu.Kwenye mabawa huchukua Watakatifu.HujaonaMahitaji kakupaAlichokiweka wakfu?

3. Sifa kwa Bwana, mlinzi akuwezeshaye.Hakika fadhila yake daima i nawe.TafakariUwezo wa Mwenyezi,Rafiki akupendaye.

4. Sifa kwa Bwana! O! Nafsi yangu umwabudu!Wote ungana na Abrahamu kumwabudu!Na “amina!”Zijumlishe sifa,Sasa tunapoabudu.