Book cover

Mungu wa Baba Zetu wa Kale

Nyimbo za Dini, 35


0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Mungu wa baba zetu wa kale,Mkonowe watawala kote,Twaimba nyimbo za shukuraniMbele ya Kiti chako cha Enzi.

2. Upendowe ulituongoza;Nchi hii huru umetupa.Kuwa Mlinzi, Mlezi wetu,Njia zako ziwe njia zetu.

3. Vitisho vya vita na taabu,Mkono wako utunusuru.Dini yako safi itujae.Wema wako uturutubishe.