Book cover

Msingi Imara

Nyimbo za Dini, 36


0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Msingi imara, Watakatifu, Wajengwa kwa neno la Bwana kwenu! Aseme nini zaidi ya haya— Nani kwa Mwokozi, nani kwa Mwokozi, Nani kwa Mwokozi kakimbilia?

2. Kwa hali zozote— ugonjwa, afya, Umaskini na wingi wa neema, Barani, majini, nyumbani na ng’ambo— Zidaivyo siku, zidaivyo siku, Zidaivyo siku, kudra huavyo.

3. Msiogope kwani niko nanyi, Ni Mungu wenu, nawapa auni. Nitawaimarisha, msimame— Kwa mkono wangu, kwa mkono wangu, Kwa mkono wangu— milele yote.

4. Nikuitapo, vilindi kupita Majonzi kwako hayatafurika, Kwani niko nawe, kukubariki, Na kuzitakasa, na kuzitakasa, Na kuzitakasa, zako huzuni.

5. Majaribu ya moto upatapo, Neema yangu, itoshayo, ipo. Moto hutadhuru; nakusudia Kuzichoma taka, kuzichoma taka, Kuzichoma taka, kukusafisha.

6. Hadi uzeeni huthibitisha Upendo wangu ulioimara; Kisha, mvi zirembapo utosi, Ni mwanakondoo, ni mwanakondoo, Ni mwanakondoo mwangu moyoni.

7. Nafsi iliyotegemea Bwana Kamwe kwa adui sitoitupa; Hata jehanamu iitikise, Kamwe sithubutu, kamwe sithubutu, Kamwe sithubutu itelekezwe!