Book cover

Kwa Wema wa Dunia

Nyimbo za Dini, 42


0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Kwa wema wa dunia, Kwa uzuri wa mbingu, Kwa pendo la daima Lizungukalo kwetu.

Bwana, Muumba wetu, Twaimba kukusifu.

2. Kwa wema wa majira, Mchana na usiku, Bonde, mti na ua, Anga na zake nuru.

Bwana, Muumba wetu, Twaimba kukusifu.

3. Kwa furaha, upendo, Kaka, dada, wazazi, Marafiki wajao, Kwa mawazo mazuri.

Bwana, Muumba wetu, Twaimba kukusifu.