1. Twamjia Bwana kuomba baraka; Hukanya, hutupa mapenzi yake; Sasa wasumbufu wakoma maovu. Bwana tumsifu; Yu na waja wake.
2. Yu nasi kutuongoza, Mungu wetu, Falme kuitunza na kustawisha; Siku hadi siku vita tumemudu; Bwana, upo nasi; Tukuzwa daima!
3. Tunakusifu, kiongozi mshindi, Na tunaomba utuhami tena. Tuepushe sote na adui yule. Usifiwe juu! Tuhurishe Bwana!