Book cover

Angazia

Nyimbo za Dini, 46


0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Niangaze kwenye giza hili.Niongoze!Ni usiku, na nyumbani mbali;Niongoze!Nioneshe njia ya kupitaHata hatua moja yatosha.

2. Sikuwa hivi, na sikuombaNiongozwe.Nilipenda njia zangu; sasa,Niongoze!Nilipenda raha, bila hofu,Nisamehe kwa kiburi changu.

3. Umenibariki na hakikaUpo nami—Kwenye mito, mabonde, milima,Na mauti.Na kukicha nitatabasamu,Na wapendwa, wale wafu wangu!