1. Ninakuhitaji, Ewe Bwana. Hakuna mwingine Kuniponya.
Yesu nakuhitaji; Muda wote Bwana! Nibariki Mwokozi; Naja kwako!
2. Ninakuhitaji; Kwangu njoo. Jaribu hushindwa Ukiwepo.
Yesu nakuhitaji; Muda wote Bwana! Nibariki Mwokozi; Naja kwako!
3. Ninakuhitaji, Muda wote. Njoo kwa haraka, Niwezeshe.
Yesu nakuhitaji; Muda wote Bwana! Nibariki Mwokozi; Naja kwako!
4. Ninakuhitaji, Bwana Mungu. Nifanye wa kwako, Mtukufu!