Book cover

Mwokozi, Niongoze

Nyimbo za Dini, 52


0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Mwokozi, niongoze Dhoruba niipite; Mawimbi yanizonga, Hatari zajificha. Mwenye ramani zote, Mwokozi, niongoze.

2. Kama mwana kwa mama, Bahari watuliza; Mawimbi yakutii Usemapo “Amani!” Nahodha na Mfalme, Mwokozi, niongoze.

3. Niifikapo pwani, Kufura kwa mawimbi Kwatisha pumziko; Naegamia kwako, Nasikia wasema, “Tulia; Naongoza.”