Book cover

Bwana, Dhoruba Yavuma

Nyimbo za Dini, 53

0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Bwana, dhoruba yavuma! Mawimbi ni makali! Na giza limetanda mbingu. Hifadhi ipo mbali. Hujali twaangamia? Walalaje foo, Hali kila dakika yatisha Na tishio la kifo?

Upepo, mawimbi yaitika: Nyamaza. Ghadhabu ya tufani, iwe Pepo chafu, watu au chochote, Hakuna maji ya kumdhuru Bwana wa bahari, nchi, mbingu. Vyote vitakuitikia: Nyamaza, tulia. Vyote vitakuitikia: Tulizana.

2. Bwana, kwa majonzi mengi Leo nanyenyekea. Moyo umejaa taabu. Niokoe, naomba! Mabubujiko ya dhambi Yalemea roho, Nafa maji! Nazama! Ee Bwana. Ninyoshee mkono!

Upepo, mawimbi yaitika: Nyamaza. Ghadhabu ya tufani, iwe Pepo chafu, watu au chochote, Hakuna maji ya kumdhuru Bwana wa bahari, nchi, mbingu. Vyote vitakuitikia: Nyamaza, tulia. Vyote vitakuitikia: Tulizana.

3. Bwana, vitisho vyakoma. Hali sasa tulivu. Jua la akisi ziwani, Moyoni sina hofu. Kawia, Bwana mpendwa! Nitoe upweke, Nifikie bandari ya kheri Pwani nipumzike.