Book cover

Nachungwa na Bwana

Nyimbo za Dini, 54


0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Nachungwa na Bwana; sikosi kitu. Nalishwa pazuri; nina amani. Naongozwa penye maji tulivu, Kwake sipotei na sinyanyaswi, Kwake sipotei na sinyanyaswi.

2. Nipoteapo kwenye bonde la kifo, U Mlezi wangu, sihofu mwovu. Nitaimarishwa na fimbo yako. Sidhuriki kama upo karibu. Sidhuriki kama upo karibu.

3. Nipatwapo na dhiki, nina chakula. Kikombe chajaa baraka tele. Wanipaka kichwa changu mafuta. Nini zaidi ya hayo niombe? Nini zaidi ya hayo niombe?