Book cover

Njoo kwa Yesu

Nyimbo za Dini, 59


0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Njoo kwa Yesu, ulemewaye, Usumbukaye nazo dhambi, Akuongoze upumzike Kwao wenye imani.

2. Njoo kwa Yesu, atakupata Japo gizani, mpotevu. Upendo wake utaongoza Ufike kwenye nuru.

3. Njoo kwa Yesu, atasikia, Ukimuomba pendo lake. Je unajua na malaika Wako karibu nawe?

4. Njoo kwa Yesu, kila taifa, Katika ulimwengu huu. Kwetu wote wa hii dunia, Aita “Njoo kwangu.”