1. Nyenyekea ushindwapo, Bwana atakuongoza,Atakuongoza na kuyajibu maombi.Nyenyekea uombapo, Bwana atakubariki,Atakubariki kwani hakika hujali.
2. Nyenyekea kwenye wito, Bwana atakufundisha,Kutumikia watu, kwa pendo la upole.Nyenyekea tamanio, Bwana atakufikisha,Atakufikisha uishi naye milele.