Book cover

Nipe Uongofu

Nyimbo za Dini, 64


0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Nipe uongofu, Nijutie dhambi, Nipe stahamala, Nijitahidi, Nipe uelewa Nidhamirie. Nipe ukarimu Nihudumie.

2. Nipe shukurani Nisimsahau, Nipe moyo safi Nimuabudu, Nipe sikitiko, Nilie Naye, Nipe usikivu, Nimtukuze.

3. Nipe utakaso, Mbinguni nifike, Nipe na usafi, Dhambi nishinde. Nipe ustahili, Mwenye kufaa. Nipe utukufu— Ulivyo Bwana.