Book cover

Kristo Mwokozi

Nyimbo za Dini, 66


0:00 0:00
Introduction
All Verses

1. Kristo Mwokozi ni Mfalme! Naimba kwa moyo wote; Kwa furaha nitasifu, Niseme amina kuu. Kristo Mwokozi; ndiye Neno. Aliishi kati yao, Alifanya miujiza Tulisifu lake jina.

2. Kristo Mwokozi; ndiye Bwana! Alikuja kutawala Kati yao, wanadamu, Na dhambi awanusuru. Kristo Mwokozi; ndiye nija. Karithi yote ya Baba, Asema: “Njooni kwangu, Na ninyi muwe na Mungu.”

3. Kristo Mwokozi — Bwana, Mungu! Neno lake lina nguvu. Nitamwabudu kwa dhati; Ndiye chanzo cha ukweli. Kristo Mwokozi ni dhamana. Kwa Shetani hunitoa. Nitaishi kwa upendo Kule mbinguni alipo.

4. Kristo Mwokozi ni Muumba! Kwake ndoto natimiza; Nipitapo kwenye dhiki, Ye husema: “Utastawi.” Kristo Mwokozi niwe naye Siku hiyo, kwa vyovyote, Akija kwa walimwengu Kutawala kati yetu.